IQNA

Jinai za Israel

Hizbullah  yaiambia Israel: Hatuogopi wala haturudi nyuma

19:54 - September 19, 2024
Habari ID: 3479454
IQNA - Afisa mwandamizi wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kusimama kidete harakati hiyo ya muqawama katika kuilinda nchi hiyo dhidi ya vitendo vya hivi karibuni vya kichokozi vya utawala wa Kizayuni.

Sayed Hashem Safieddine, mkuu wa Halmashauri Kuu ya Hizbullah pia aliahidi kwamba Hizbullah italipiza kisasi kwa utawala huo.

"Tutasema hivi kwa adui wa Kizayuni kwamba hatutaogopa wala hatutarudi nyuma," alisema.

"Tunawaonya makamanda wote wa jeshi la adui kwamba muqawama uko tayari," aliongeza, akizungumza wakati wa hafla ya mazishi ya wanachama wa harakati hiyo, ambao waliuawa shahidi wakati wa operesheni dhidi ya adui Mzayuni.

"Kila mtu anapaswa kuhakikisha kuwa muqawama una nguvu ya juu, na unaweza kusababisha mapigo mazito kwa adui," afisa huyo alibainisha.

Matamshi yake yametolewa siku moja baada ya milipuko kuwalenga wanaotumia kifaa cha mawasiliano cha Pager kote Lebanon na kupelekea watu takriban watu 14 kupoteza maisha wakiwemo watoto wawili, na kuwajeruhi karibu wengine 3,000.

Pager ni kifaa cha mawasiliano ya simu kisichotumia waya ambacho hupokea na kuonesha jumbe za alphanumeric au sauti.

"Hakika tutajibu tukio hili la kigaidi," afisa wa Hezbollah alisisitiza.

Baadaye siku ya Jumatano, takriban watu 20 zaidi walipoteza maishana wengine zaidi ya 450 kujeruhiwa baada ya vifaa zaidi vya mawasiliano kulipuka kote Lebanon, ikiwa ni pamoja na katika mji mkuu Beirut pamoja na kusini na mashariki mwa nchi hiyo.

Utawala wa Israel umekataa kutoa maoni yoyote kuhusu matukio hayo, lakini Hizbullah imeishikilia kuwa inawajibika kikamilifu.

Tukio la Jumatano lilikuwa baya zaidi kulenga Lebanon tangu Oktoba 7, wakati utawala huo wa kigaidi ulipoanzisha mashambulizi yake mabaya dhidi ya Lebanon kutokana na hatua ya Hizbullah kutekeleza operesheni za kijeshi za utawala huo ili kuunga mkono Wapalestina wa Gaza.

 

3489959/

Habari zinazohusiana
Kishikizo: lebanon hizbullah israel
captcha